Psalms 91:3-8


3 aHakika yeye ataniokoa na mtego wa mwindaji,
na maradhi ya kuambukiza ya kuua.

4 bAtakufunika kwa manyoya yake,
chini ya mbawa zake utapata kimbilio,
uaminifu wake utakuwa ngao na kinga yako.

5 cHutaogopa vitisho vya usiku,
wala mshale urukao mchana,

6 wala maradhi ya kuambukiza
yanayonyemelea gizani,
wala tauni iharibuyo adhuhuri.

7 Ijapo watu elfu wataangukia kando yako,
kumi elfu mkono wako wa kuume,
lakini haitakukaribia wewe.

8 dUtatazama tu kwa macho yako
na kuona adhabu ya waovu.

Copyright information for SwhKC